Pata taarifa kuu

Marekani: Watu wanane wafariki baada ya boti mbili kuzama kwenye pwani ya California

Watu wanane walikufa maji baada ya kuzama kwa boti mbili ndogo "za magendo" usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili karibu na jiji la San Diego, California, mamlaka ya eneo hilo imesema.

Mhamiaji kutoka Haiti akipumzika kabla ya kujaribu kuvuka mpaka wa Marekani akitokea Mexico mnamo Septemba 21, 2021 huko Mexico.
Mhamiaji kutoka Haiti akipumzika kabla ya kujaribu kuvuka mpaka wa Marekani akitokea Mexico mnamo Septemba 21, 2021 huko Mexico. © AP/Fernando Llano
Matangazo ya kibiashara

 

"Hii ni moja ya mikasa mbaya zaidi ya magendo ya baharini huko California ninayojua," amesema James Gartland, afisa wa idara ya huduma za dharura wa San Diego, akionekana kurejelea wimbi la wahamiaji kati ya Mexico na Marekani. Waathiriwa ni watu wazima, ameongeza, bila kutaja uraia wao.

Wito wa kuomba msaada ulitolewa karibu saa tano na nusu usiku siku ya Jumamosi na mtu anayezungumza Kihispania, ambaye alisema watu 15 walikuwa kwenye boti moja na wanane kwenye nyingine. Walipofika eneo la tukio, waligundua kuwa "boti mbili zilipinduka", alisema Bw. Gartland.

Waokoaji "hawakupata manusura wowote" wakati wa operesheni zao, lakini watu waliweza kufika ufukweni na "kuondoka ufukweni", Bw Gartland amesema. Eneo ambalo boti hizo zilikuwa "ni eneo la hatari, hata mchana kweupe", ni eneo lenye mikondo mikali, amebaini.

Jiji la San Diego liko karibu sana na mpaka kati ya Mexico na Marekani. Wahamiaji wengi huvuka mpaka kinyume cha sheria, suala ambalo ni usumbufu wa kisiasa kwa utawala wa Rais Joe Biden. Wahamiaji, ambao wanataka kuepuka umaskini au vurugu katika nchi zao za asili, mara nyingi huchukua hatari kubwa kuingia katika ardhi ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.