Pata taarifa kuu

Washington yatangaza kuipatia Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot

Marekani itaipatia Ukraine mfumo wake wa hali ya juu zaidi wa ulinzi wa anga, Patriot, mkuu wa diplomasia ya Marekani ametangaza siku ya Jumatano, Desemba 21, 2022, wakati ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipokuwa anakaribia kutua Washington. 

Makombora ya Patriot yanaonekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Rzeszow-Jasionka, Machi 25, 2022, huko Jasionka, Poland. Marekani itatuma msaada wa kijeshi wa dola bilioni 1.8 kwa Ukraine.
Makombora ya Patriot yanaonekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Rzeszow-Jasionka, Machi 25, 2022, huko Jasionka, Poland. Marekani itatuma msaada wa kijeshi wa dola bilioni 1.8 kwa Ukraine. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

"Msaada wa leo unajumuisha kwa mara ya kwanza mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot, wenye uwezo wa kurusha makombora ya cruise, makombora ya masafa mafupi ya balestiki na ndege katika miinuko ya juu zaidi kuliko ulinzi wa mifumo ambayo ilikuwa imetolewa hadi sasa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Maekani Antony Blinken amesema katika taarifa.

Volodymyr Zelensky amewasili Marekani. Rais wa Ukraine atakutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden mjini Washington, kabla ya kuhutubia Bunge la Congress.

Vladimir Putin, Rais wa Urusi, ameweka malengo ya jeshi la Urusi kwa mwaka wa 2023: Urusi itapeleka kambi za jeshi la majini huko Mariupol na Berdiansk, meli ya kikosi hiki itakuwa na kombora mpya la hypersonic, idadi ya jeshi itaongezeka kwa wanajeshi milioni 1.5, utatu wa nyuklia umewekwa kwenye hali ya kusubiri.

Serikali ya Urusi imegawanyika katika kuanzisha mashambulizi makubwa ya majira ya baridi, kulingana na Marekani.

Wakati ukarabati bado unaendelea, Ukraine inahofia mashambulizi zaidi dhidi ya miundombinu yake ya nishati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.