Pata taarifa kuu

Jeshi la Urusi lataka kuongeza idadi ya wanajeshi wake hadi milioni 1.5

Wakati wa mkutano na maafisa wakuu wa jeshi siku ya Jumatano, Vladimir Putin ameahidi kuendelea kukuza uwezo wake wa kijeshi na kuvipa vikosi vya jeshi la Urusi njia zote muhimu kwa operesheni yao nchini Ukraine, hasa kwa kuongeza idadi ya wanajeshi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa hotuba yake kwa hadhira ya maafisa wa jeshi Jumatano, Desemba 21, 2022 mjini Moscow.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa hotuba yake kwa hadhira ya maafisa wa jeshi Jumatano, Desemba 21, 2022 mjini Moscow. © Mikhail Kuravlev / AP
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii, Desemba 21, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema ni 'muhimu' kuongeza idadi ya wanajeshi katika jeshi la Urusi hadi wanajeshi milioni 1.5, katikati ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine. Pia amependekeza kuongeza kikomo cha umri kwa huduma ya kijeshi, "kuhakikisha utimilifu wa kazi ili kuhakikisha usalama wa Urusi".

Mbele ya maafisa wakuu wa jeshi la Urusi, Rais Vladimir Putin ameelezea "makubaliano" yake na mapendekezo haya, akihakikisha kwamba maendeleo haya yatafanyika "bila uharibifu" kwa jamii na uchumi wa nchi. Tayari mnamo mwezi Agosti, agizo la rais lilibaini kuongeza idadi ya wanajeshi hadi milioni 1.15 ifikapo Januari 1, 2023.

Kuimarisha safu ya jeshi la Urusi

Wakati wa mkutano huu unaopaswa kuanzisha malengo ya jeshi la Urusi kwa mwaka wa 2023, mkuu wa Kremlin amesisitiza nia yake ya kuendelea kuimarisha uwezo wake wote wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na "utayari wa kupambana" wa vikosi vyake vya nyuklia. Kulingana na matangazo yake, meli za Urusi zitakuwa na makombora mapya ya Zicron hypersonic cruise tangu mwanzoni mwa mwezi Januari, "ambayo hayafanani au kuwa na uwezo wa makomorayoyote duniani", amebaini. Rais wa Urusi pia amesisitiza umuhimu wa ndege zisizo na rubani katika mzozo na Ukraine.

Tutaendelea kuvipa vikosi vyetu vya kimkakati na silaha za hali ya juu. Narudia: mipango yetu yote itatekelezwa, kwa njia fulani. Tutaendelea kudumisha na kuboresha utayari wa kupambana na utatu wetu wa nyuklia.

Vladimir Putin na matangazo yake kwa jeshi la Urusi

Sergei Shoigu wakati huo huo amedai kupeleka kambi za jeshi la majini kusaidia meli zake katika miji miwili inayokaliwa kwa mabavu ya Ukraine, Mariupol na Berdiansk. Kwa sababu hakika ni moja ya "vipaumbele" vilivyotajwa wakati wa hotuba hii: "kuendelea kutekeleza operesheni maalum [nchini Ukraine] hadi majukumu yake yote yametimizwa", kama ilivyotangazwa na waziri wa ulinzi.

Mzozo wa Ukraine, 'janga la kawaida'

Baada ya kutoa pongezi kwa muda mfupi kwa wanajeshi wa Urusi waliouawa vitani, Vladimir Putin ameuita mzozo wa Ukraine 'janga la kawaida', bila hata hivyo kuwajibika kwa kuzuka kwake au athari zake.

Kulingana na rais, nchi hiyo itaweza kuendelea kufadhili kampeni yake ya kijeshi bila matatizo, licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi. "Nchi na serikali hutoa kila kitu ambacho jeshi linaomba. Kila kitu kabisa! "Amesema kiongozi wa Urusi, ambaye mnamo mwezi Septemba aligiza uhamasishaji wa kijeshi baada ya vikwazo vya kimkakati katika mzozo huo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.