Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron azuru Washington

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anawasili Washington jioni ya Novemba 29 na kuanza ziara ya kiserikali ya siku mbili Jumatano asubuhi, na ataendelea hadi New Orleans siku ya Ijumaa. Hii ni ziara ya pili ya serikali nchini Marekani kwa rais wa Ufaransa, ambaye tayari alikuwa amealikwa na Donald Trump mwezi Aprili 2018. "Heshima" ambayo Élysée imekaribisha wakati ambapo Emmanuel Macron anataka kuchukua fursa ya kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na Marekani.

Joe Biden na Emmanuel Macron, Oktoba 29, 2021 huko Roma.
Joe Biden na Emmanuel Macron, Oktoba 29, 2021 huko Roma. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza ya kiserikali ya kwa ofisi ya rais wa Marekani Joe Biden na rais Emmanuel Macron ndiye ananufaika na ziara hii. Katika ikulu ya Élysée, hawatusiti kukumbusha ili kuonyesha umuhimu wa tukio hilo, hasa kwa vile Emmanuel Macron pia ni rais wa kwanza wa Ufaransa kualikwa mara mbili na Washington katika ziara ya kiserikali, kiwango cha juu cha itifaki, ishara ya kutambuliwa ambayo ni "nadra na kuthaminiwa", kulingana na wasaidizi wa rais wa Jamhuri ambao wanasifu uhusiano "wa kipekee " kati ya Ufaransa na Marekani. Uhusiano ambao hata hivyo ulikuwa na hali mbaya wakati Australia ilipovunja mkataba muhimu na Ufaransa kwa ajili ya ununuzi wa manowari kwa manufaa ya Washington.

Ushirikiano mpya wa "transatlantic"

Tangu wakati huo,  Emmanuel Macron anafanya ziara hii kwa nia ya kuunganisha "ushirikiano mpya wa transatlantic" ambao ni kutokana na athari ya vita vya Ukraine na kuhakikisha Ulaya nafasi katika mashindano ya ulimwengu , haswa na China. 

Suala la ukaribu

Akiwa na Joe Biden, Emmanuel Macron, kwa sasa, amecheza kadi ya mahusiano ya kibinafsi chini ya alivyofanya na Donald Trump, hata kama wasaidizi wake wanaelezea uhusiano wa "mzuri na wa kirafiki". Mjini Washington, moja ya changamoto kwa Emmanuel Macron itakuwa pia kuonyesha ukaribu wake na rais wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.