Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: Mkakati wa Ufaransa barani Afrika 'utakamilika ndani ya miezi sita'

Mkakati mpya wa Ufaransa barani Afrika utakamilika ndani ya miezi sita baada ya mashauriano na washirika wake katika bara hilo, Rais Emmanuel Macron ametangaza Jumatano, kuthibitisha kumalizika kwa Operesheni Barkhane, kikosi kilioundwa mnamo mwaka 2014, kwa minajili ya kupambana dhidi ya wanajihadi, kaskazini na magharibi mwa Afrika. 

"Hatuna nia ya kubaki kwa muda usiojulikana kwenye uwanja wa operesheni", amebainisha Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake huko Toulon.
"Hatuna nia ya kubaki kwa muda usiojulikana kwenye uwanja wa operesheni", amebainisha Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake huko Toulon. © Eric Gaillard, Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Katika siku zijazo, tutazindua awamu ya mazungumzo na washirika wetu kutoka Afrika, washirika wetu na mashirika ya kikanda ili kukuza kwa pamoja hadhi, muundo na misheni ya kambi za sasa za jeshi la Ufaransa huko Sahel na Afrika Magharibi," rais wa Ufaransa amesema wakati akiwasilisha mkakati mpya wa ulinzi wa Ufaransa. “Mkakati huu utakamilika ndani ya miezi 6 (...). Ni muhimu na ni moja ya athari ambayo tunapata kutokana na yale ambayo tumepitia katika miaka ya hivi karibuni katika eneo lote la Sahel,” alieleza.

"Hatuna nia ya kubaki kwa muda usiojulikana kwenye uwanja wa operesheni", amebainisha Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake huko Toulon.

Uinguliaji wetu kati lazima uwe na kikomo bora kwa wakati," ameongeza. "Hii ndiyo sababu nilichukua uamuzi, kwa uratibu na watendaji wengine, kusitisha Operesheni Barkhane".

"Ushirikiano wetu una maana ikiwa ni wa kweli na unajibu mahitaji ya wazi ya majeshi ya Afrika, ikiwa unasaidia ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutawala katika nchi hizi".

"Lazima tujue namna ya kubadili mbinu, dhamira yetu na nchi za Afrika lazima ijikite katika mantiki ya uungaji mkono na ushirikiano, ndiyo maana tutazindua awamu ya mazungumzo na washirika wetu wa Afrika, ili kuendeleza hadhi na misheni ya kambi za Ufaransa, barani Afrika", rais amebaini.

Urasimishaji huu unakuja miezi mitatu baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali. Baada ya kuongezeka kwa ukosoaji dhidi ya vikosi vya Ufaransa na mamlaka ya kisiasa ya ya nchi hiyo, rais wa Ufaransa alitangaza mwezi wa Februari mwaka huu kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa waliokwenda kusaidi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.