Pata taarifa kuu

Marekani: Biden 'hana nia ya kuketi kwenye meza ya maungumzo na' Putin katika G20

Rais wa Marekani amefutilia mbali mkutano wowote wa nchi mbili na mwenzake wa Urusi kabla ya mkutano wa kilele wa G20 uliopangwa kufanyika mwezi wa Novemba nchini Indonesia.

Rais wa Marekani afutilia mbali mkutano wowote wa nchi mbili na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Marekani afutilia mbali mkutano wowote wa nchi mbili na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House imesema siku ya Alhamisi kwamba Rais wa Marekani Joe Biden "hana na nia" ya kufanya mazungumzo katika mkutano wa nchi mbili na Vladimir Putin katika mkutano wa kundi la nchi tajiri duniani, G20, ambao viongozi hao wawili wanatarajiwa kuhudhuria mwezi ujao wa Novemba huko Bali, Indonesia.

Biden "hana nia ya kufanya mazungumzo" na mwenzake wa Urusi, msemaji mkuu wa masuala ya usalama wa taifa John Kirby amesema. Bwana Biden pia alitangaza kuwa "hana nia" ya kukutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman katika  kikao cha G20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.