Pata taarifa kuu

Saudi Arabia yatoa msaada wa kibinadamu wa dola milioni 400 kwa Ukraine

Jumla ya dola milioni 400 ni kiasi cha misaada ya kibinadamu ambayo Saudi Arabia imetoa kwa Ukraine. Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky walikuwa na mazungumzo ya simu kuhusu suala hilo. Ishara inayoonyesha kwa mara nyingine tena msimamo maalum - na wenye utata - wa ufalme dhidi ya wahusika wa vita nchini Ukraine.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammad bin Salman (picha yetu) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky walikuwa na mazungumzo ya simu kuhusu kifurushi cha msaada wa kibinadamu cha dola milioni 400.
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammad bin Salman (picha yetu) na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky walikuwa na mazungumzo ya simu kuhusu kifurushi cha msaada wa kibinadamu cha dola milioni 400. AFP - HO
Matangazo ya kibiashara

"Kuunga mkono kila kitu kitakachochangia kupunguza mgogoro wa kivita", ni kwa maneno haya ambapo Saudi Arabia inahalalisha utoaji wa msaada huu wa kibinadamu kwa Ukraine. Msaada huu unatolewa wakati ambapo kunaripotiwa mvutano kamili kati ya Ryad na Washington.

Saudi Arabia, kwa hakika, imekataa kufungua milingoti ya uzalishaji wa mafuta. iliedelea kusalia kimya na kutosikia maombi kutoka kwa Merika ambayo iliitaka Ryad kuchukua hatua ili kupunguza athari za mgogoro wa nishati. Uamuzi huo ulichukuliwa ndani ya mfumo wa OPEC +, ambayo Urusi pia ni mwanachama. Urusi ambayo, kama wazalishaji wengine wa mafuta, lazima wanufaike na matengenezo ya bei ya "dhahabu nyeusi".

"Athari"

Katika muktadha huu, je, dola milioni 400 za msaada wa kibinadamu kwa Ukraine zitatosha kutuliza hasira za wale wote wanaoituhumu Saudi Arabia yenye ushirikiano na Moscow? Hakuna uhakika wowote kwa hilo. Rais wa Marekani ameahidi kutokea kwa "athari mbaya" kwa kile Saudi arabia "wamefanya na Urusi".

Saudi arabia - kwa upande wake - imefutilia mbali ukosoaji wa Marekani na kubaini kwamba uamuzi wake ulichukuliwa kwa msingi wa mazingatio ya kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.