Pata taarifa kuu

Visa vya watu kutoweka vyakithiri Mexico

Tarehe 30 Agosti 2022 ni siku ya kimataifa ya kukumbuka manusura na waathirika wa vitendo vya kutoweshwa duniani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, mkakati huu wa kikatili wa kutisha raia ni tatizo la kimataifa, lakini nchini Mexico, ambako watu 100,000 wametoweka tangu 1964, inaleta sura mbaya kwa nchi tangu mwaka 2014 na suala la kutoweka kwa wanafunzi 43 bado halijapatiwa ufumbuzi.

Ndugu wa wahanga wameshikilia mabango yenye picha za wanafunzi waliotoweshwa wakati wa maandamano ya kudai haki katika Jiji la Mexico, Agosti 26, 2022.
Ndugu wa wahanga wameshikilia mabango yenye picha za wanafunzi waliotoweshwa wakati wa maandamano ya kudai haki katika Jiji la Mexico, Agosti 26, 2022. REUTERS - HENRY ROMERO
Matangazo ya kibiashara

Mnamo 2021, kamati dhidi ya vitendo vya kutoweshwa ambayo iko ziarani nchini Mexico imesema ina wasiwasi juu ya hali inayojiri nchini Mexico na hali ya unyanyasaji inayoathiri waathiriwa na familia zao katika muktadha ambapo wahusika hawaadhibiwi. Miongoni mwa watu waliotoweka, kuna wanafunzi 43 wa Ayotzinapa, waliotekwa nyara usiku wa Septemba 26 kuamkia Septmba 27, 2014. Jambo hili lililozua sintofahamu nchini Mexico na ufichuzi mpya wa hivi majuzi ambao unaonyesha kuwa kesi hiyo ni "uhalifu wa serikali" inaendelea kutikisa Mexico juu ya tatizo hili sugu. Miaka minane baadaye, mabaki ya miili ya wanafunzi watatu pekee kati ya 43 ndiyo yamepatikana.

Akija kusaidia familia wakati wa maandamano ya kutafuta haki, Juventina Nicolas, kutoka shirika linalopambana dhidi ya mateso na kutokujali, amesisitiza: Utafiti na uchunguzi havipaswi kusitishwa.

“Hii ni miaka minane ya maandamano, utafiti, mateso kwa wazazi kwa huzuni mkubwa kwa sababu bado hakuna haki. Tunachotaka ni wapi kujua walipo! Wako wapi ? amesema Juventina Nicolas.

"Vita hivi ambavyo Felipe Calderon alivianzisha mwaka wa 2006 na ambavyo vilileta wimbi hili zima la umwagaji damu na kutoweka kwa watu kote Mexico vilituathiri sote moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja", anaeleza Angelica Orozco, mmoja wa wajumbe wa shirika linalotetea haki kwa wahanga waliotoweka. Shirika letu linaambatana na familia kukabiliana na kutojali na kutochukua hatua kwa mamlaka. Kwa sababu mara nyingi ni ndugu wenyewe ambao huchunguza na kutafuta kupotea kwao. “Lengo letu siku zote litakuwa kuwatafuta. Tunaweza kuona kwamba si polisi wala tume ya utafiti ya ndani yenye nia yoyote ya kubadilisha mambo,” amebaini.

Nchini Mexico, katika idadi kubwa ya visa vya watu kutoweshwa, hakuna mhalifu anayeadhibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.