Pata taarifa kuu

Mwandishi Salman Rushdie alazwa hospitalini baada ya kudungwa kisu jukwaani New York

Mwandishi wa Uingereza mwenye asili ya India, Salman Rushdie, ambaye kitabu chake cha riwaya alichokiita, 'Aya za kishetani' (Satanic Verses) kilisababisha kulengwa na agizo la (Fatwa) ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah nchini Iran Ruhollah Khomeini mwaka 1989, alidungwa kisu siku ya Ijumaa alipokuwa akijiandaa kutoa mhadhara. Amefanyiwa upasuaji wa dharura.

Mwandishi Salman Rushdie, hapa ilikuwa mwaka 2019 huko Vienna, alikuwa akilengwa mnamo 1989 na agizo "fatwa" la kutaka kuuawa.
Mwandishi Salman Rushdie, hapa ilikuwa mwaka 2019 huko Vienna, alikuwa akilengwa mnamo 1989 na agizo "fatwa" la kutaka kuuawa. AFP - HERBERT NEUBAUER
Matangazo ya kibiashara

Salman Rushdie alikuwa karibu kuzungumza katika ukumbi wa michezo wa Taasisi ya Chautauqua kwenye tamasha la fasihi la kifahari, wakati mtu mmoja aliharakia jukwaani na kumpiga mwandishi na mhojiwaji wake. Picha za video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakikimbia kumsaidia mtu aliyelala chini. Watu waliondolewa haraka katika eneo hilo.

Mwandishi huyo wa fasihi mwenye umri wa miaka 75 alipangiwa kuzungumzia uhuru wa wasanii mbele ya hadhara ya mamia ya watu, alipovamiwa na mtu aliyefunika uso kwa barakowa, ambaye alimshambulia kwa visu.

Polisi wa Jimbo la New York inasema Salman Rushdie alidungwa kisu "angalau mara moja" shingoni na "angalau mara moja" kwenye tumbo. Mwandishi huyo alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali ya eneo hilo ambako amefanyiwa upasuaji. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wake Andrew Wylie ametangaza kwamba anapumulia mashine hospitalini na kwamba amejeruhiwa vibaya: "Habari sio nzuri. Salman anaaminika kupoteza jicho, mishipa ya fahamu kwenye mkono wake ilikatika, na alidungwa kisu kwenye ini, ambalo limeharibika. Mhojiwa kwa upande wake alipata jeraha kidogo kichwani.

Mshukiwa ametambuliwa kama Hadi Matar, 24, kutoka Fairview, New Jersey. Mapema mchana, mwendo wa saa 10.47 asubuhi (saa za New York), Salman Rushdie alikuwa amewasili jukwaani kwa ajili ya mkutano huo wakati mshukiwa alipopanda jukwaani na kumvamia Bw Rushdie. Alimchoma kisu angalau mara moja shingoni na tumboni. Polisi wa jimbo hilo wanasaidiwa katika uchunguzi huu na ofisi ya Sharif na pia FBI. Katika hatua hii, bado hakujapatikana maelezo kamili juu ya sababu kamili za mshukiwa.

Ni kutoka jamii ya Kashmir

Rushdie alizaliwa mjini Mumbai, India katika familia ya Kiislamu kutoka Kashmir, lakini alihamia Uingereza. Maisha yake yalibadilika baada ya kuandika kitabu cha riwaya alichokiita, Satanic Verses, maana yake, Aya za kishetani, ambacho Waislamu wengi walikishutumu kuwa na maandishi yanayomkashifu Mtume Muhammad na kuukufuru Uislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.