Pata taarifa kuu

Marekani kutuma vikosi vya kijeshi Ulaya Mashariki

Rais wa Marekani Joe Biden anapanga kutuma vikosi vya kijeshi Ulaya Mashariki kusaidia vikosi vya NATO, afisa mkuu wa utawala wa Marekani amesema Jumatano wiki hii, huku vyombo vya habari vya Marekani vikitaja idadi hiyo kuwa ya wanajeshi 3,000.

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. Nicholas Kamm AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani imetangaza Jumatano Februari 2 kutumwa kwa wanajeshi 3,000 wa ziada wa Marekani katika Ulaya Mashariki ili kuzilinda nchi za NATO "dhidi ya uchokozi wowote", wakati ambapo nchi za Magharibi zinazidisha maonyo kwa Urusi kwamba wanashuku kwamba inataka kuivamia Ukraine.

"Kulingana na maagizo ya rais na kwa mujibu wa mapendekezo ya waziri wa Ulinzi Lloyd James Austin, wizara itaweka upya hasa katika Mashariki baadhi ya vitengo vilivyoko Ulaya", afisa huyo mkuu wa Marekani amebaini, bila kutaja idadi.

"Vikosi hivi havitapigana nchini Ukraine," amebaini. "Harakati hizi sio za kudumu, zinajibu kwa hali ya sasa." Maelfu ya wanajeshi hawa watatumwa tena kutoka Ujerumani kwenda Romania, na wengine 2,000 watatumwa kutoka kambi kubwa ya Marekani ya Fort Bragg, North Carolina, kwenda Ujerumani na Poland, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.