Pata taarifa kuu

Covid-19 Marekani: Idadi ya watoto wagonjwa yaongezeka katika Jimbo la New York

Wengi wanajiuliza iwapo kirusi kipya cha Omicron kinaambukiza zaidi kwa watoto kuliko kile cha awali? Tangu katikati ya mwezi Desemba, Marekani imeshuhudia ongezeko la zaidi ya 30% la kulazwa kwa watoto hospitalini kwa sababu ya Covid-19.

Katika wiki mbili, idadi ya watoto wagonjwa wa Covid waliolazwa hospitalini imeongezeka mara nne.
Katika wiki mbili, idadi ya watoto wagonjwa wa Covid waliolazwa hospitalini imeongezeka mara nne. AFP - SPENCER PLATT
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya afya ya Jimbo la New York,nchini Marekani ambayo imeguswa na hali hiyo imetangaza kwamba wanafuatilia hali hii inayotia wasiwasi.

Kulazwa kwa watoto hospitalini kwa sababu ya Covid-19 bado ni ya tukio la kipekee, kulingana na majimbo, hali hii ni 2% hadi 4 tu ya waliolazwa kwa jumla. Lakini hali iliyorekodiwa huko New York imesababisha mamlaka kutahadharisha, kwani katika wiki mbili, idadi ya watoto wagonjwa wa Covid waliolazwa hospitalini imeongezeka mara nne.

Kati ya watoto hawa, hakuna hata mmoja aliyepata chanjo kamili. Ni lazima kusema kwamba nusu ya waliolazwa hospitalini ni watoto walio na umri ulio chini ya miaka 5, ambao bado hawajastahiki chanjo.

Vijana walio na dalili za hatari

Katika ngazi ya kitaifa, Marekani imerekodi ongezeko la 31% katika siku kumi. Kwa wastani, wiki iliyopita watoto 800 kwa siku walilazwa katika hospitali nchini Marekani. Kulingana na Gazeti la Washington Post, wengi ni vijana walio na dalili za hatari.

Jumatatu hii, Desemba 27, kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi nchini Marekani na uhaba wa vipimo, Rais Joe Biden aliwatolea wito Wamarekani akiwataka wasiwe na hofu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.