Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Takriban watu 50 wafariki dunia katika mlipuko wa lori

Watu wasiopunguwa 50 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kulipuka mapema Jumanne huko Cap-Haitien, nchini Haiti, mlipuko ambao pia umesababisha watu wengi kujeruhiwa, kulingana na ripoti ya awali iliyotolewa na afisa wa eneo hilo.

Cap-Haitien, eneo kuliko tokea kisa cha lori kulipuka na kusababisha maafa makubwa.
Cap-Haitien, eneo kuliko tokea kisa cha lori kulipuka na kusababisha maafa makubwa. AFP/HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

“Niliona kati ya watu 50 na 54 wakiteketea kwa moto wakiwa hai katika eneo la tukio. Ni vigumu kuwatambua, "amesema naibu meya wa Cap-Haitien, Patrick Almonor.

"Takriban nyumba 20" zinazopatikana karibu naeneo la tukio pia ziliwaka moto kufauatia mlipuko huo, Almonor amebaini, na kuzua hofu ya kuongezeka kwa idadi ya watu waliofariki dunia.

"Bado hatujaweza kutoa maelezo kuhusu idadi ya wahanga katika nyumba hizo," almesema.

Nchi hii inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta, kutokana na kujihusisha kwa magenge kwenye sehemu ya mzunguko wa mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.