Pata taarifa kuu

Marekani: Jaji wa Shirikisho azuia kwa muda sheria inayokataza utoaji mimba huko Texas

Jaji wa jimbo la Texas nchini Marekani, amezuia kwa muda utekelezwaji wa sheria inayozuia uviaji mimba.Sheria hii ilianza kutekelezwa kuanzia tarehe Septemba 1, kuzuia uaviaji mimba, wakati mapigano ya moyo ya mtoto yanapoanza kusikika.

Makumi ya maelfu ya wanawake waliandamana huko Marekani kutetea haki ya kutoa mimba Oktoba 2, 2021.
Makumi ya maelfu ya wanawake waliandamana huko Marekani kutetea haki ya kutoa mimba Oktoba 2, 2021. Sergio FLORES AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo inatoa nafasi kwa yeyote lkwenda Mahakani kufungua kesi dhidi ya yeyote aliyesaidia utoaji wa mimba na anaweza kupewa tuzo ya Dola Elu 10.

Mara nyingi, wakati uja uzito una wiki sita, wasichana na wanawake wengi huwa hawafahamu iwapo ni wajawazito.

Jaji huyo ameagiza kutotekelezwa, kwa sheria hiyo baada ya kuomba idhini kutoka kwa rais Joe Biden, kwa kile alichosema, kuna madai kuwa, sheria hiyo inakwenda kinyume  na Katiba ya Marekani.

Katika miaka ya hivi karibuni, sheria kama hizi zimepitishwa katika baadhi ya majimbo lakini haikutekelezwa kwa sababu inakwenda kinyume na Katiba ya Marekani.

Mahakama ya Juu nchini Marekani mwaka 1973, iliamua kuwa utoaji mimba unaweza kufanyika nchini humo na haki kwa wanawake kutoa mimba ambayo haijafika wiki 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.