Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Antony Blinken ziarani Paris katikati mwa mvutano kati ya Ufaransa na Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken yuko ziarani katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, kuhudhuria mkutano wa OECD, na anatarajia kukutana na mwenzake wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, Septemba 23, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, Septemba 23, 2021. REUTERS - EDUARDO MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya  Antony Blinken inalenga kuboresha maridhiano na Ufaransa baada ya mgogoro wa kidiplomasia wa hivi karibuni, kufuatia hatua ya Australia kuvunja mkataba wa nyambizi za Ufaransa na kufikia mkataba na Marekani.

Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Antony Blinken, ambaye anazungumza Kifaransa, atakuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na viongozi mbalimbali wa Ufaransa.

Antony Blinken anaichukulia Paris, ambapo aliishi kwa kipindi cha miaka kumi akiwa kijana, kama "makaazi yake ya pili"

Kwa kupenda Ufaransa tangu ujana wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alipokelewa furaha kwa katika mji mkuu wa Ufaransa wakati wa ziara yake mwezi Juni maka huu.

Lakini hali imebadilika. Tangazo la kushtukiza la ushirikiano katika ukanda wa Indo-Pacific na hatua ya Australia ya kuvunja mkataba wa ununuzi wa nyambizi za Ufaransa na hivyo nchi hiyo kufikia mkataba mpya na Marekani kumesababisha mgogoro ambao haujawahi kutokea kati ya nchi hizo mbili. Kulingana na Gazeti la New York Times, Wafaransa wanashindwa kuelewa ni kwanini Antony Blinken hakuwaambia kuhusu maandalizi ya mapatano haya na Australia na Uingereza wakati alipotembelea nchi hiyo mwezi Juni mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.