Pata taarifa kuu
SAHEL-USALAMA

Sahel: Marekani yaahidi kuimarisha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Marekani Joe Biden walikutana Jumatano, Septemba 22, 2021, ili kujieleza baada ya mgogoro uliosababishwa na kuvunjika kwa makubaliano kuhusu nyambizi za Australia.

Kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa Chad wakati wa mazoezi ya pamoja "Flintlock" mnamo mwaka 2015.
Kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa Chad wakati wa mazoezi ya pamoja "Flintlock" mnamo mwaka 2015. REUTERS/Emmanuel Braun
Matangazo ya kibiashara

Ili kupunguza mvutano, Marekani ilibaini katika ya pamoja na ikulu ya Élysée, "kwamba wamejitolea kuimarisha ushirikiano wao kwa operesheni za kupambana na ugaidi" zinazoongozwa na Umoja wa Ulaya katika ukanda wa Sahel. Hii ni hatua mpya ya ushirikiano ambao umedumu kwa zaidi ya miaka nane.

Uwepo wa jeshi la Marekani ni muhimu, na ushirikiano huo ni wa zamani, kwani Washington imekuwa upande wa Ufaransa tangu kuanza kwa Operesheni Serval mnamo mwaka 2013. Marekani vile vile ilichangia kwa msaada katika vifaa na zaidi ya yote kwa suala la ujasusi, ISR, "ujasusi," ufuatiliaji na utambuzi ".

Pia kuna uchukuzi wa kimkakati. Kwa jumla, 20% ya abiria na 10% ya usafirishaji wa ndani husimamiwa na jeshi la anga la Marekani. Marekani pia inatoa msaada wa mafuta kwa ndege kwa 40%, hali ambayo inawezesha ndege za kivita za Ufaransa kufanya operehseni zake za angani katika eneo nzima.

Lakini msaada muhimu zaidi ni ujasusi, kwa hivyo ni muhimu kuwakabili wanjihadi. Kuna usaidizi mwingine wa Marekani kwa kufanya ukaguzi wa eneo hilo kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizoko Niger huko Agadez na Niamey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.