Pata taarifa kuu
UN-USHIRIKIANO

Guterres atoa wito kwa Washington na Beijing kufanya mazungumzo

Mjadala mkuu wa kikao cha 76 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umeanza Jumanne, Septemba 21, kwa hotuba ya Katibu Mkuu Umoja wa mataifa, Antonio Guterres, ambaye amezitolea wito Marekani na China kuketi kwenye meza ya "mazungumzo" na kuwa waelewa ".

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye kikao cha 76 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 21, 2021.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye kikao cha 76 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 21, 2021. AP - Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya Marekani na China dhidi ya uharibifu zaidi wa dunia ambao unaripotiwa kwa sasa. Antonio Guterres ametoa wito wa kufayika kwa mazungumzo kati ya Washington na Beijing, hasa katika eneo linalochunguzwa na kutamaniwa zaidi kwa sasa: ukanda wa Indo-Pacific.

Ametaka kuonya juu ya hatari ya dunia kugawanyika kwa kambi mbili katika mvutano kati ya China na Marekani. "Tunakabiliwa na mtafaruku mkubwa wa mizozo ya maisha yetu," amebainisha. Nina hofu kwamba dunia yetu inaelekea kugawanyika mara mbili kwa tofauti za sheria za kiuchumi, biashara, kifedha na teknolojia, njia mbili tofauti katika ukuzaji wa ujasusi bandia, na mwishowe, mikakati miwili tofauti ya kijeshi na kijiografia. "

"Tunahitaji kuwa na mazungumzo. Tunahitaji ufahamu. Lazima tuwekeze katika kuzuia, kudumisha na kutunza amani. Tunahitaji maendeleo katika upunguzaji wa silaha za nyuklia na katika juhudi zetu za kawaida za kupambana na ugaidi. Tunahitaji vitendo vilivyojikita katika kuheshimu haki za binadamu, " amesisitiza Antonio Guterres.

Wakuu wa nchi na serikali  zaidi ya mia moja wapo New York licha ya janga la Covid-19, na pia mawaziri kadhaa.

Wakati huo rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alikuwa akiongea kwa mara ya kwanza mbele ya Mkutano Mkuu wa Umoja w Mataifa, katikati ya mgogoro wa manowari amesema. "Hatutafuti vita vipya baridi au ulimwengu uliogawanywa katika kambi tofauti," lakini Marekani itatetea nafasi yake duniani "kwa nguvu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.