Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA

Marekani yaondoa vizuizi kwa wasafiri wa kimataifa

Marekani itawaruhusu watu wote kutoka nchi za kigeni kuingia nchini Marekani kuanzia mwezi Novemba kwa sharti kwamba wamepewa chanjo kamili dhidi ya Covid, Ikulu ya White House imetangaza Jumatatu hii Septemba 20.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Newark huko New Jersey, Marekani, Novemba 25, 2020.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Newark huko New Jersey, Marekani, Novemba 25, 2020. REUTERS - MIKE SEGAR
Matangazo ya kibiashara

Miezi 18 baada ya kutangazwa na utawala wa Trump mwezi Machi 2020, marufuku ya kuingia nchini Marekani kwa wasafiri wa kimataifa hatimaye itaondolewa. Raia watakao ruhusiwa kuingia nchini Marekani ni kutoka nchi 33, ikiwa ni pamoja na zile za Umoja wa Ulaya, Uingereza na China.

Lakini ufunguzi huu wa mipaka utaambatana na masharti magumu, ameonya mratibu wa mapambano dhidi ya janga la Covid katika ikulu ya White House, Jeff Zients. Wasafiri watalazimika kuonyesha uthibitisho wa chanjo dhidi ya Covid-19, kufanya vipimo ndani ya siku tatu kabla ya safari yao kwenda Marekani na kuvaa barakoa.

Chanjo zipi?

Ikulu ya White, hata hivyo, haikutaja mara moja ni chanjo zipi zitawezesha kuingia kwenye ardhi ya Marekani. Hili haliwezi kulezeka kwani, hata hivyo, Waingereza na raia kutoka nchi Umoja wa Ulaya wengi wamepokea chanjo ya AstraZeneca, ambayo haitambuliki nchini Marekani, Marekani inatambua tu chanjo za Pfizer / BioNTech, Moderna na Johnson & Johnson. (Janssen). Na Chibna inatumia chanjo yake iliyotengeneza kama Urusi.

"Hii inawahusu watu wote waliopewa chanjo ambazo zinatambuliwa na mamlaka ya Dawa nchini Marekani", amebaini Kamishna wa Ulaya Thierry Breton, anayehusika na kuratibu usambazaji wa chanjo za kupambana na Covid na ambaye alizungumza na mratibu wa janga la Covid katika Ikulu ya White House. "Aliniambia kuwa kwa chanjo zingine, hasa AstraZeneca, ni mamlaka yao ya afya ambayo itaamua, lakini alionekana kuwa  mtu mwenye matumaini," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.