Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA

Ripoti iliyoombwa na Biden juu ya chimbuko la Covid-19 haijahitimishwa

Ripoti iliyoombwa na rais wa Marekani Joe Biden kutoka kwa idara yake ya ujasusi juu ya chimbuko la Covid-19 haiwezeshi suala hili nyeti kutatuliwa, ikiwa ndio chanzo cha mvutano kati ya Washington na Beijing, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Rais wa Marekani Joe Biden aliipa idara yake ya ujasusi siku 90 ili kutoa ripoti kuhusu chimbuko la Covid-19.
Rais wa Marekani Joe Biden aliipa idara yake ya ujasusi siku 90 ili kutoa ripoti kuhusu chimbuko la Covid-19. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Mishoni mwa mwezi Mei rais wa Marekani alitoa wito kwa idara ya ujasusi ya Marekani, ambayo hadi sasa hawezi kutoa uamuzi juu ya chinmbuko hili ikiwa linatokana na wanyama au kuvuja kwa maabara ya China huko Wuhan, "kuongeza juhudi zao" ili kuelezea chimbuko la Covid-19 na kutoa ripoti ndani kipindi cha siku 90.

Siku ya Jumanne Bw. Biden alipokea ripoti hiyo ambayo ilikuwa imewekwa siri lakini ripoti yenyewe haijahitimishwa kwa sababu licha ya utafiti na uchambuzi wao, maafisa wa ujasusi hawakuweza kuafikiana juu ya ufafanuzi dhahiri, kulingana na Gazeti la Washington Post ambalo limenukuu maafisa wawili wa Marekani walio karibu na faili hiyo.

Hii inaelezwa kwa sehemu moja kwamba China haijatoa taarifa za kutosha, limesema Gazeti la Wall Street Journal,Β  pia likinukuu maafisa wakuu wawili wa Marekani.

Kulingana na maafisa walionukuliwa na Gazeti la Washington Post, idara ya ujasusi itajaribu katika siku zijazo kupunguza sehemu za ripoti hiyo ili kutolewa kwa umma.

China, ambayo inapinga vikali nadharia ya maabara, inashutumu Washington kwa kueneza habari za uongo ili kupiaka matope.

Janga la Covid-19 limewauwa watu wasiopungua 4,439,888 duniani kote tangu mwishoni mwa mwezi Desemba 2019, kulingana na ripoti iliyotolewa Jumanne wiki hii na shirika la habari la AFP kutoka vyanzo rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.