Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFYA

Biden aahidi kubambana dhidi ya COVID-19 katika ukanda wa Pasifiki

Rais wa Marekani Joe Biden amewaambia viongozi wa nchi zinazoshiriki Mkutano wa Visiwa vya Pasifiki kwamba watapewa dozi za chanjo dhidi ya COVID-19 zilizotolewa na Marekani bila masharti ya kisiasa.

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. AP - Matt Rourke
Matangazo ya kibiashara

Katika miaka ya hivi karibuni, China imesisitiza matarajio yake katika ukanda wa Pasifiki, na kusababisha Marekani na washirika wake kuonya mataifa ya visiwa vya ukanda huo juu ya hatari ya kuchukuwa madeni ya Beijing. China imeendelea kusema kuwa itaendeleza uhusiano na mataifa ya Pasifiki kwa kuheshimiana na kwa usawa.

Joe Biden amesema katika Mkutano wa Visiwa vya Pasifiki kwamba Marekani itatoa mchango wa "nusu bilioni" wa chanjo iliyotengenezwa na maabara ya Pfizer kwa pango wa kimataifa wa ugawaji chanjo, COVAX, ambayo sehemu yake itatumwa katika ukanda wa Pasifiki.

"Hatuweki masharti yoyote juu ya dozi hizi - ni juu ya kuokoa maisha," Joe Biden ameuambia mkutano huo unaofanyika mkondoni, unaowashirikisha viongozi kutoka nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Fiji, Papua New Guinea, 'Australia na New Zealand.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.