Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani yaongeza muda wa uvaaji wa barakoa katika sekta ya uchukuzi

Utawala wa Marekani umetangaza kuwa una mpango wa kuongeza muda wa kuvaa barakoa kwa watu wanaosafiri kwa ndege, treni na mabasi na vile vile katika viwanja vya ndege na vituo vya treni hadi Januari 18 ili kuzuia hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Wakati aina mpya ya kirusi cha Corona, kinachoambukiza zaidi, kinaendelea kuenea nchini Marekani, utafiti unaonyesha kuwa kuvaa barakoa mbili ni kinga bora dhidi ya maambukizi.
Wakati aina mpya ya kirusi cha Corona, kinachoambukiza zaidi, kinaendelea kuenea nchini Marekani, utafiti unaonyesha kuwa kuvaa barakoa mbili ni kinga bora dhidi ya maambukizi. AFP - KENA BETANCUR
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Utawala wa Usalama wa Usafiri (TSA) amethibitisha uamuzi huo, na kuongeza kuwa "lengo la maagizo haya ni kupunguza kuenea kwa janga la Corona katika sekta ya uchukuzi wa umma".

Hatua hii ya kuongeza muda wa kuvaa barakoa katika sekta ya uchukuzi inaonyesha kuwa kuna hatari ya kusambaa kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, Delta, kinachosambaa haraka, na inaonyesha kuwa sekta ya uchukuzi wa umma inaendelea kuwa hatari, hasa kwa watu ambao hawajachanjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.