Pata taarifa kuu
CUBA-SIASA

Rais wa Cuba ahoji vikwazo vya Marekani kwa kuunga mkono maandamano

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel amelaaani vikwazo vya Marekani, ambavyo vimeongezwa katika miaka ya hivi karibuni, shida za kiuchumi ambazo nchi inakabiliwa nazo, hasa na uhaba wa dawa na kukata mara kwa mara kwa umeme, kutokana na maandamano ambayo hayajawahi kutokea kwa miongo kadhaa mwishoni mwa wiki hii iliyopita.

Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel huko Havana.
Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel huko Havana. AP - Ariel Ley Royero
Matangazo ya kibiashara

Akiongea kwenye televisheni, huku akizungukwa na wajumbe wa serikali yake, kiongozi huyo wa Cuba amesema ukosoaji wa dhidi ya udhibiti wa janga la COVID-19 nchini Cuba unalenga kuvunja umoja wa wananchi wa taifa hilo.Miguel Diaz-Canel amelaani matukio ya vurugu na uporaji ambao ulifanyika katika miji kadhaa ya nchi, akishtumu tabia hiyo "mbaya kabisa ya waandamanaji, isiyo ya adabu na ya kihuni".

Rais wa Marekani Joe Biden, kwa upande wake, amewahakikishia raia wa Cuba kuwa Marekani inawaunga mkono mbele ya kile alichoonyesha kama miongo kadhaa ya ukandamizaji na usimamizi usiofaa kabisa wa mgogoro wa kiafya unaosababishwa na janga la COVID-19.

"Raia wa Cuba kwa ujasiri wanadai haki za kimsingi zinazokubalika kimataifa. Haki hizi, pamoja na haki ya kuandamana kwa amani na haki ya kuchagua kwa uhuru mustakabali wa nchi yao, lazima ziheshimiwe," amesema katika taarifa.

"Marekani inatoa wito kwa utawala wa Cuba kuwasikiliza raia wake na kukidhi mahitaji yao kwa wakati huu muhimu kuliko kujitajirisha."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.