Pata taarifa kuu
CUBA-SIASA

Washington yaonya Cuba juu ya matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji

Washington imeonya Cuba dhidi ya matumizi yoyote ya nguvu yanachochea ghasia dhidi ya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika kote nchini humo jana Jumapili dhidi ya "udikteta".

Maandamano yalifanyika kote Cuba na hasa katika mji mkuu Havana wakidai uhuru zaidi, Jumapili, Julai 11, 2021.
Maandamano yalifanyika kote Cuba na hasa katika mji mkuu Havana wakidai uhuru zaidi, Jumapili, Julai 11, 2021. © Eliana Aponte/AP
Matangazo ya kibiashara

"Marekani inaunga mkono uhuru wa kujieleza na uhuru wa kuandamana nchini Cuba, na inalaani vikali matumizi yoyote yenye lengo la kuchochea ghasia au yanayolenga kuhatarisha maisha ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani kama haki yao kwa kudhiirisha hasira zao," Mshauri wa Usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter

Jumapili Julai 11, Cuba ilishuhudia tukio la kihistoria. Maandamano ambayo hayajawahi kutokea yalishuhudiwa nchi nzima. Kutoka Mashariki hadi Magharibi, Wacuba walionyesha hasira zao wakiandamana, huku wakiomba "uhuru" na kulaani "utawala wa kiimla". Maandamano yamekuwa yakipigwa marufuku katika kisiwa hicho, kinachotawaliwa na Chama pekee cha Kikomunisti kwa miongo kadhaa.

"Karibu katika mikoa yote na katika miji kadhaa, watu wameingia mitaani kwa sababu tumechoshwa na shida hizi! », mmoja wa waandamanaji hao amesema.

"Hapa tuna njaa". "Tunataka tu kuandamana kwa amani na kuonyesha uhuru wetu, lakini polisi wawanakabiliana na mtu yeyote anayethubutu kuandamana!" », mwandamanaji mwengine amebaini. "Hii ni mara ya kwanza tunaandamana kwa idadi ubwa ya watu, lakini haiyatakuwa maandamano ya mwisho! », ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.