Pata taarifa kuu
CUBA-CORONA-AFYA

Cuba yaudhibiti ugonjwa wa Covid-19

Kwa wiki mbili zilizopita, watu wengi wamepona virusi vya Corona nchini. Lakini ili kuepuka wimbi la pili la mlipuko huo, kisiwa hiki kimezindua kampeni kubwa ya vipimo, kwa hofu ya kuongezeka visa vingi vya maambukizi kwenye foleni za watu wakati wa kununua chakula.

Watu wakiwa kwenye foleni wakati wa kununua chakula huko Havana, Mei 13, 2020.
Watu wakiwa kwenye foleni wakati wa kununua chakula huko Havana, Mei 13, 2020. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kati ya Aprili 26 na Mei 13, visa vipya 473 vya maambukizi vilivyothibitishwa viliripotiwa nchini humo na wagonjwa 889 wameopona virusi hivyo kwa kipindi hicho.

Siku ya Jumatano, kesi sita pekee zilijiongeza, kwa wagonjwa 49 waliopona na jumla ya kesi 1,810 za maambukizi zilizoripotiwa tangu kuanza kwa janga hilo, ikiwa ni pamoja na vifo 79.

Cuba nchi yenye wakazi milioni 11.2, sasa ina kesi 403 tu za maambukizi. Hata hivyo mamlaka nchini humo imebaini kwamba kutokana na juhudi hizo za kukabiliana na janga la Covid-19 haiwezi kusema kuwa ni ushindi kwa nchi hiyo.

"Takwimu hizi, tunazitoa kwa uangalifu sana, ili tusiweze kuwapa moyo raia kwamba tatizo sasa limeisha," amesema Daktari Francisco Duran, mkurugenzi wa idara ya kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukia kwenye Wizara ya Afya, anayehusika na kutoa takwimu hizo kila siku kwenye televisheni.

Kufungwa kwa mipaka na shule, kuweka karantini watu ambao wamekutwa na virusi vya Corona, kwatafuta watu wenye dadili za ugonjwa wa Covid-19 nyumba kwa nyumba: Huo ndio mkakati wa mamlaka nchini Cuba dhidi ya Corona.

Na " kutokana na hatua hizo matokeo yake ni kwamba, wagonjwa wengi wanapona kuliko kesi mpya!", amesema mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Cuba, José Moya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.