Marekani: CDC yaagiza uvaaji wa barakoa katika maeneo yanayokumbwa na COVID
Maafisa wa afya nchini Marekani wametangaza hatua mpya ya uvaaji wa barakoa kwa watu waliopewa chanjo kamili dhidi ya COVID, wakisema ni bora kuendelea kuvaa barakoa katika maeneo yaliyofungwa katika majimbo ya Marekani ambapo Corona inaendelea kusambaa kwa kasi.
Imechapishwa:
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Vituo vya Udhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC) wamesema kituo hicho kimeagiza walimu na wanafunzi wote, bila kujali hali yao ya chanjo kuvaa barakoa.
Pia wametoa wito kwa mamlaka husika kushinikiza raia kupata chanjo na kuvaa barako ili kuzuia kuenea zaidi kwa janga la Corona katika maeneo ambapo kiwango cha maambukizi kiko juu.