Pata taarifa kuu
MAREKANI-COVID 19

Biden awaambia Wamarekani kuendelea kupambana na janga la Covid 19

Rais wa Marekani Joe Biden katika maadhimisho ya sikukuu ya uhuru Julai 4 amewaambia Marekani kuwa nchi hiyo bado haijashinda vita dhidi ya virusi vya corona, licha ya serikali yake kuendeleza mapambano kwa utoaji wa chanjo.

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Marekani Julai  4 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Marekani Julai 4 2021. REUTERS - EVELYN HOCKSTEIN
Matangazo ya kibiashara

Akizugumza mbele ya watu 1, 000 katika Ikulu ya White House, Biden amesema njia pekee ya kushinda maambukizi hayo ni kwa wananchi wa Marekani kuendelea kupokea chanjo.

Msinielewe vibaya, janga la Covid 19 halijakwisha. Tunafahamu kuwa kuna aina mpya wa virusi inayoitwa Delta, lakini ulinzi mzuri ni kupata chanjo.

Katika hotuba yake, Biden alitoa heshima kwa watu zaidi ya 600,000 waliopoteza maisha kutoka na janga la Corona kuanzia mwaka 2020.

Mpaka sasa, ni asilimia 46 ya Wamarekani ndio waliopokea dozi kamili ya kuzuia maambukizi hayo.

Marekani ina maambukizi zaidi ya Milioni 33.7 na ndio nchi ya kwanza iliyoathiriwa na maambukizi haya duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.