Marekani: Idara za ujasusi zapitisha nadharia mbili juu ya chimbuko ya COVID-19
Makao makuu ya Upelelezi nchini Marekani imesema kwamba mashirika yake yana nadharia mbili juu ya chanzo cha janga la COVID-19, idara mbili zinaweka mbele nadharia ya kuibuka kwa asili kupitia mawasiliano ya kibinadamu na wanyama wenye virusi vya Corona, idara ya tatu ikitetea nadharia ya ajali inayowezekana ya maabara.
Imechapishwa:
"Mashiria ya ujasusi ya Marekani hayana uhakika ni wapi, lini, au jinsi virusi vya COVID-19 vilipitishwa mwanzoni, lakini yamekusanya karibu matukio mawili," ofisi ya mkurugenzi wa ujasusi katika ngazi ya kitaifa imesema.
Idara nyingi inaamini kwamba kuna "habari za kutosha kukadiria uwezekano mmoja zaidi kuliko mwingine," imeongeza.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano aliomba idara za ujasusi za Marekani kumpa ripoti juu ya chimbuko cha janga hilo ndani ya siku 90.