Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Waziri Mkuu mpya wa Haiti aahidi kurejesha utulivu na kuandaa uchaguzi

Waziri Mkuu mpya wa Haiti Ariel Henry alichukua madaraka rasmi Jumanne katika nchi inayokabiliwa na machafuko, akiahidi kurejesha utulivu ili kuandaa uchaguzi unaohitajika na raia wa nchi hiyo na jamii ya kimataifa.

Kaimu waziri mkuu, Claude Joseph (kushoto), na Waziri Mkuu mpya wa Haiti Ariel Henry (kulia).
Kaimu waziri mkuu, Claude Joseph (kushoto), na Waziri Mkuu mpya wa Haiti Ariel Henry (kulia). VALERIE BAERISWYL AFP
Matangazo ya kibiashara

Ariel Henry, 71, ni Waziri Mkuu wa saba na wa mwisho aliyeteuliwa na rais Jovenel Moïse, ambaye aliuawa na kundi la watu wenye silaha Julai 7.

"Moja ya mambo muhimu ninayotakiwa kutekeleza kwa sasa, ninawahakikishia wananchi kwamba tutafanya kila linalowezekana kurejesha utulivu na usalama. Hili ni moja wapo ya mambo makuu ambayo rais wa Jamhuri alinitaka nifanye kwa sababu alielewa kwamba ilikuwa hatua ya lazima ikiwa tutafanikiwa hatua nyingine ya kuandaa uchaguzi wa kuaminika, huru, na wa wazi, "Bwana Henry alisema.

Serikali mpya, ambayo ilichapishwa Jumatatu katika jarida rasmi la Jamhuri ya Haiti, inaundwa na mawaziri 18, wakiwemo wanawake watano. Mbali na wadhifa wa Waziri Mkuu, Ariel Henry atachukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Jamii na Kazi.

Claude Joseph, ambaye alikuwa Kaimu Waziri Mkuu wakati wa mauaji ya rais na alitaka yeye ndiye achukuwe nafasi waziri mkuu, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ibada.

Mvutano kati ya Bw. Joseph na Ariel Henry kuchukua nafasi ya waziri mkuu, hatimaye ulipatiwa suluhu mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya shinikizo la pamoja lililotolewa na mabalozi kutoka nchi tofauti, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Marekani, wajumbe wa jumuiya ya mataifa ya Amerika (OAS) na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.