Pata taarifa kuu
BRAZIL-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi nchini Brazil yapindukia milioni 15

Brazil imerekodi visa vipya 73,380 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya siku ya Alhamisi, ikifanya jumla ya idadi ya maambukizi nchini kufikia zaidi ya milioni 15 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Vifo vipya 2,550 kutokana na COVID-19 vimerekodiwa katika muda wa saa ishirini na nne, na kufikisha vifo 416,949 nchini Brazil.
Vifo vipya 2,550 kutokana na COVID-19 vimerekodiwa katika muda wa saa ishirini na nne, na kufikisha vifo 416,949 nchini Brazil. REUTERS - AMANDA PEROBELLI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, vifo vipya 2,550 kutokana na COVID-19 vimerekodiwa katika muda wa saa ishirini na nne, kwa na kufikisa vifo 416,949.

Hayo yanajiri wakati Urusi, Ufaransa na Ujerumani zinaunga mkono chanjo ya COVID-19 kuondolewa haki miliki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin pia amesema anaunga mkono juhudi hizo kuhusiana na chanjo inayotengenezwa nchini mwake.

Akizungumza katika mkutano ulioonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni, Rais Putin amesema wanasikia mawazo yanayotoka Umoja wa Ulaya ambayo kwa mtazamo wake yanafaa kusikilizwa, na ameitaka serikali yake kutakafari uwezekano wa kuondoa haki miliki kwa chanjo ya Urusi dhidi ya virusi vya corona, Sputnik V.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.