Pata taarifa kuu
BRAZIL-UISALAMA

Brazil: Ishirini na tano wauawa katika operesheni dhidi ya madawa ya kulevya Rio

Takriban watu 25, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi, waliuawa Alhamisi (Mei 6) katika operesheni kubwa dhidi ya madawa ya kulevya katika eneo moja huko Rio de Janeiro, vyombo vya habari vya Brazil vimeripoti

Operesheni ya polisi dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya huko Jacarezinho katika jimbo la Rio de Janeiro, Brazil, Mei 6, 2021.
Operesheni ya polisi dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya huko Jacarezinho katika jimbo la Rio de Janeiro, Brazil, Mei 6, 2021. AFP - MAURO PIMENTEL
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ilifanywa mapema Alhamisi dhidi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wanaotuhumiwa kuajiri watoto wadogo katika kitongoji duni cha Jacarezinho, kaskazini mwa mji wa Rio, tovuti ya habari ya G1 imeripoti, ikinukuu polisi. Televisheni ya GloboNews imerusha hewani picha zinazoonyesha watu wenye silaha wakikimbia wakati wa operesheni ya polisi.

Wakazi pia wamekuwa wakirusha video kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha milipuko, milio ya risasi na helikopta zikiruka juu ya eneo hilo.

Watu walalamikia ukatili uliofanywa

Idadi kubwa ya polisi walionekana wakizunguka kitongoji hicho. Wakaazi walisikia milio ya risasi kutoka pande zote. Kulikuwa na hofu kubwa, kama alivyosema wakili wa haki za binadamu Maria Julia Miranda akiongea na mwandishi wetu Martin Bernard. "Huu ni ugaidi kabisa katika eneo hili… Jambo la kwanza linaloumiza ni kiwango cha damu unachoweza kuona katika eneo hili, kulimeonekana damu nyingi zikitapakaa ardhini. Katika nyumba ya kwanza tuliyotembelea, familia ilifukuzwa, kijana mmoja aliuawa katika chumba cha kulala cha msichana wa miaka nane. Familia iliona ukatili huu. Mtoto huyu ameumizwa sana na kitendo hiki cha kikatili. "

Afisa wa polisi aliuawa katika operesheni hiyo. Lakini watu wengine waliouawa hawakuta hawakutajwa. "Leo, tunaona ushahidi wa tisa, kwa mara nyingine tena, kwamba hakuna sheria katika vitongoji vya Rio", amesema Joel Luiz da Costa, mtu anayesimamia Taasisi ya Ulinzi ya watu Weusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.