Pata taarifa kuu
BRAZILI

Brazili: Mahakama Kuu yaidhinisha kufutwa kwa hukumu ya Lula

Majaji wengi wa Mahakama Kuu nchini Brazil wameidhinisha uamuzi wa hapo awali kutoka Mahakama ya Juu zaidi nchini humo ikithibitisha kufutwa kwa hukumu za jinai zilizokuwa zinamkabili rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva.

Rais wa zamani wa Brazil Lula wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Machi 10 huko Sao Paulo.
Rais wa zamani wa Brazil Lula wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari. Machi 10 huko Sao Paulo. REUTERS - AMANDA PEROBELLI
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Brazil ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, ikibaini kwamba hukumu ya Lula inapaswa kuthibitishwa ili kuhifadhi "usawa wa kiutaratibu na uhakika wa kisheria".

Pamoja na hatua hiyo, Lula ykuko huru kuwania katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, ambao huenda akachuana na rais wa sasa kutoka mrengo wa kulia Jair Bolsonaro.

Kiongozi huyo wa zamani wa Chama cha Wafanyakazi (PT) alitoa hotuba mwezi uliopita ambayo ilifanana na uzinduzi wa kampeni za uchaguzi.

Lula ndiye anapewa nafasi kubwa kati ya wapinzani wa Jair Bolsonaro kukabiliana na kiongozi huyo wa mrengo wa kulia mnamo mwaka 2022. Kura za kwanza zinaonyesha kuwa kinyang'anyiro hiki kinakaribia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.