Pata taarifa kuu
BRAZIL

Brazil: Wakuu wa jeshi wajiuzulu katikati ya mzozo wa kisiasa

Miaka 57 iliyopita, jeshi lilikuwa likichukua mamlaka nchini Brazil. Tukio lililokumbukwa katika mazingira ya kipekee Jumanne, Machi 30, tangu makamanda watatu wa jeshi kujiuzulu baada ya Waziri wa Ulinzi kufutwa kazi na Rais Bolsonaro, ambaye anashukiwa kutaka kulifanya jeshi kuingia katika masuala ya kisiasa.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Juni 11, 2019.
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Juni 11, 2019. EVARISTO SA AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Katika barua yake ya kujiuzulu, Waziri wa Ulinzi, Jenerali Azevedo alisisitiza umuhimu wa "kuliweka jeshi kama taasisi ya serikali". Ukosoaji ambao wengi wanaona kuwa rais Bolsonaro anataka kulifanya jeshi kuingilia katika masuala ya siasa.

Jair Bolsonaro hapo awali alikuwa ametaka kuuawa kwa mkuu wa  jeshi la nchi kavu, Jenerali Pujol, ambaye anaunga mkono hatua za kukabiliana na janga la janga  la COVID-19. Hatimaye, aliwafukuza kazi viongozi wa majeshi matatu - jeshi la nchi kavu, jeshi la anga na jeshi la majini - hata kabla hawajajiuzulu.

Bolsonaro anatarajia kutoa ahadi kwa vyama vya mrengo wa kulia ili kutaka kuendelea kumuunga mkono.

Rais wa Brazil pia anataka kuhamasisha jeshi "lake" kupambana dhidi ya hatua za kukabiliana na janga la COVI-19, zilizowekwa katika baadhi ya majimbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.