Pata taarifa kuu
Brazili

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 90,000 zaripotiwa kwa siku moja Brazil

Brazil imerekodi visa vipya 90,303 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya coronavirus kwa siku moja, kulingana na takwiumu wilizotolewa Jumatano wiki hii na Wizara ya Afya.

Mgonjwa wa Covid-19 akisubiri kusafirishwa na ndege ya jeshi katika uwanja wa ndege wa Manaus, Brazil, Januari 15, 2021.
Mgonjwa wa Covid-19 akisubiri kusafirishwa na ndege ya jeshi katika uwanja wa ndege wa Manaus, Brazil, Januari 15, 2021. AFP - MICHAEL DANTAS
Matangazo ya kibiashara

Rekodi hii mpya inakuja siku moja baada ya idadi kubwa zaidi ya vifo vya kila siku vilivyosababishwa na COVID-19 kuripotiwa.

Ripoti za hivi karibuni zinabaini kwamba mgogoro wa kiafya katika nchi hii ya Amerika Kusini sasa umesababisha karibu watu milioni 11.7 kuambukizwa virusi vya Corona na vifo 284,775, baada ya vifo vipya 2,648 kuripotiwa kwa siku moja.

Hayo yanajiri wakati shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema watalaamu wake wangali wanatathmini data za usalama kwenye chanjo ya Covid-19 ya kampuni ya AstraZeneca kufuatia hofu ya kuganda kwa damu mwilini lakini likapendekeza kuwa mipango ya utoaji chanjo iendelee.

Wakati mamilioni ya dozi za chanjo hiyo yamekwishatolewa, idadi ndogo ya watu wamekumbwa na tatizo la kuganda damu mwilini, hali iliyozilazimu nchi yakiwemo mataifa makubwa matatu ya Umoja wa Ulaya -- Ujerumani, Ufaransa na Italia -- kusitisha kwa muda utoaji chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.