Pata taarifa kuu
BRAZILI-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Vifo vipya 721 vyaripotiwa Brazil katika muda wa saa 24

Brazil imerekodi vifo vipya 721 vinavyohusiana na COVID-19 na kesi mpya 34,027 zilizothibitishwa jana Jumapili, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya.

Watu kutoka jamii ya Muraswakiitikiwa zoezi la kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19, katika moja ya vitongoji vya Manaus, mji mkuu wa jimbo la Brazil la Amazonas, Januari 7, 2021.
Watu kutoka jamii ya Muraswakiitikiwa zoezi la kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19, katika moja ya vitongoji vya Manaus, mji mkuu wa jimbo la Brazil la Amazonas, Januari 7, 2021. AP - Edmar Barros
Matangazo ya kibiashara

Wizara hiyo inabaini kwamba visa vimepungua kidogo baada ya siku tano mfululizo zilizogubikwa na vifo visivyopungua 1,300 na visa 60,000 vya maambukizi ya kila siku.

Brazil imerekodi jumala ya vifo 254,942 vinavyohusishwa na janga hilo tangu ugonjwa huo kuzuka nchini humo.

Hayo yanajiri wakati Marekani Jumamosi Februari 27 iliidhinisha chanjo ya kampuni ya Jonhson & Johnson kwa matumizi ya dharura, na kuipatia nchi hiyo chanjo ya tatu ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona ambavyo vimeua watu 500,000 nchini humo.

Mamlaka ya chakula na dawa, FDA, imethibitisha  kuwa chanjo ya Johnson&Johnson itatolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi.

Kuidhinishwa kwake kunaongeza nguvu kwenye kampeni ya taifa ya utoaji chanjo nchini Marekani ambayo ilisuasua kwa wiki kadhaa.

Karibu raia milioni 47.2 wa Marekani tayari wamepatiwa dozi ya kwanza ya chanjo ya corona, kulingana na taasisi ya kupambana na magonjwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.