Pata taarifa kuu
BRAZIL

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yavuka milioni 6 Brazil

Brazil inakabiliwa na mlipuko wa pili wa virusi vya Corona baada ya idadi ya visa vya maambukizi kuvuka kizingiti cha visa milioni mbili vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi hivyo jana Ijumaa, Wizara ya Afya imetangaza.

Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil.
Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wana hofu ya kutokea kwa mlipuko wa pili wa virusi vy Corona nchini humo.

Marekani na India ni nchi pekee ambazo hadi sasa idadi ya visa vya maambukizi imevuka kizingiti hiki cha kesi milioni sita zilizothibitishwa.

Pamoja na karibu vifo 170,000, Brazil imetoa ripoti ya pili ya vifo vingi duniani baada ya Marekani, ambapo inazidi vifo 250,000.

Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil.

Katika miji mikubwa, maisha yamerudi katika wiki za hivi karibuni kama ilivyo kuwa kabla ya janga hilo, pamoja na baa, mikahawa na maduka yakijaa wateja, ambao mara nyingi hawavai barakoa.

Katika miji ya Rio de Janeiro na Sao Paulo, hii imesababisha katika siku za hivi karibuni kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa COVID-19 ambao hulazwa hospitalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.