Pata taarifa kuu
BRAZIL-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 12,000 vyathibitishwa Brazil

Brazil imerekodi visa vipya 12,342 vilivyothibitishwa vya virusi vya Corona na vifo vipya 290 vilivyohusishwa na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema.

Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo.
Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo. REUTERS/Bruno Kelly
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vya maambukizi nchini Brazili inazidi milioni 5.0, na jumla ya vifo 150,488 sasa vimerekodiwa, kulingana na takwimu za serikali.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.