Pata taarifa kuu
BRAZIL-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya karibu 42,000 vyathibitishwa Brazil

Brazil imerekodi visa vipya 41,906 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, sawa na rekodi ya kila siku tangu Septemba 11, Wizara ya Afya imebaini.

Raia wa Brazili waandamana huko São Paulo dhidi ya usimamizi mbaya wa Covid-19, Agosti 7, 2020.
Raia wa Brazili waandamana huko São Paulo dhidi ya usimamizi mbaya wa Covid-19, Agosti 7, 2020. REUTERS/Washington Alves
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu za serikali, zaidi ya visa milioni 4.92 vya maambukizi vimerekodiwa nchini tangu kuzuka kwa janga hilo.

Maafisa wa afya pia wameripoti vifo vipya 819, na kufanya jumla ya vifo kufikia 147,494.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.