Coronavirus: Zaidi ya vifo vipya 1,000 vyaripotiwa Brazil
Brazil imerekodi vifo vipya 1,031 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema.
Imechapishwa:
Kulingana na takwimu hizi za serikali, idadi ya vifo imeongezeka hadi 143,952 nchini kote.
Mamlaka ya afya pia imethibitisha visa vipya 33,413 vya maambukizi, na kufanya jumla ya idadi ya maambukizi kufikia milioni 4.8.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.