Biden aidhinishwa kuchuana na Donald Trump katika uchaguzi wa urais Marekani
Joe Biden ameteuliwa rasmi na chama chake cha Democratic, kuwania urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba kupambana na rais Donald Trump.
Imechapishwa:
Wajumbe wa chama hicho kutoka majimbo yote 50 wamekuwa wakikutana kupitia njia ya video kwa sababu ya janga la Corona.
Biden ambaye anatarajiwa kuwahotubia wajumbe hao siku ya Alhamisi, amewashukuru kwa kumwidhinisha yeye pamoha na mgombea mwenza wake Kamala Harris.
Marais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton na Jimmy Carter, walimsifu Biden kuwa mtu mwenye uzoefu na uadilifu wa kuinusuru Marekani iliyoathiriwa vibaya na janga la Corona.
Kongamano hilo la siku nne, mwaka huu linafanyika kwa njia ya vidio kutokana na janga la Covid-19.
Hii ni mara ya tatu kwa Biden kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais huku mwakilishi huyo wa chama cha Democratic akionekana kuwa katika kipindi cha madiliko makubwa ikizingatiwa kwamba kampeni yake ilionekana kuwa katika hatari ya kudidimia mnamo mwezi Februari.