Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Chama cha Republican chatafautiana kuhusu pendekezo la kuahirisha uchaguzi

Viongozi wakuu wa chama cha Republican nchini Marekani wamesema hawaungi mkono mapendekezo ya rais Donald Trump, anayetaka Uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba uahirishwe.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura nchini Marekani wanatarajiwa kupiga kura kwa njia ya Posta kutokana na janga la Corona, mfumo ambao rais Trump anahofia kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru na haki.

"Mwaka 2020 kutakuwa na uchaguzi usio sahihi na wa udanganyifu zaidi katika historia," rais wa Marekani aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Alhamisi wiki hii, akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.

"Itakuwa aibu ya kweli kwa Marekani. Uchaguzi uahirishwe hadi pale watu waweze kupiga kura salama na kwa njia ya kawaida", ameongeza.

Bunge la Congress pekee ndilo lina uwezo wa kuamua juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais. Majimbo kadhaa ya Marekani yanataka uchaguzi ufanyike kwa njia ya posta ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19. Majimbo mengi yameruhusu mfumo huu wa upigaji kura kwa miaka kadhaa na hayajaripoti matatizo yoyote makubwa isipokuwa matukio madogo.

Chini ya uchaguzi wa urais, Bwana Trump hana mamlaka yoyote ya kuahirisha uchaguzi yeye binafsi na tukio kama hilo ni lazima liidhinishwe na bunge.

Bwana Trump alisema njia hiyo tayari inadhihirisha kwamba hilo litakuwa matatizo tu katika maeneo ambayo imejaribiwa.

Mapema mwezi huu, majimbo sita ya Marekani yalikuwa yanapanga kufanya uchaguzi wa Novemba kwa njia ya posta: California, Utah, Hawaii, Colorado, Oregon naWashington.

Majimbo hayo yatatuma kura moja kwa moja kwa njia ya posta kwa wapiga kura wote waliosajiliwa, na baada ya hapo zitarejeshwa tena au kuwasilishwa siku ya kupiga kura - ingawa kupiga kura moja kwa moja bado kutakuwepo kwa wachache ambao hali italazimu kufanya hivyo.

Rais Trump anatarajiwa kupambana na aliyewahi kuwa Makamu wa rais Joe Biden ambaye atapeperusha bendera ya chama cha Democratic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.