Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Mvutano waibuka Marekani baada ya Trump kupendekeza uchaguzi wa urais uahirishwe

Baada ya rais wa Marekani Donald Trump kupendekeza, kwa mara ya kwanza, uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Novemba 3 uahirishwe, akionyesha hatari za udanganyifu zinazohusiana na janga la Covid-19, pendekezo hilo limeibua mtafaruku nchini humo.

Donald Trump katika Ikulu ya White Juni 15, 2020.
Donald Trump katika Ikulu ya White Juni 15, 2020. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

"Mwaka 2020 kutakuwa na uchaguzi usio sahihi na wa udanganyifu zaidi katika historia," rais wa Marekani aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Alhamisi wiki hii, akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.

"Itakuwa aibu ya kweli kwa Marekani. Uchaguzi uahirishwe hadi pale watu waweze kupiga kura salama na kwa njia ya kawaida", ameongeza.

Uamuzi wa rais hautoshi

Bunge la Congress pekee ndilo lina uwezo wa kuamua juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais. Majimbo kadhaa ya Marekani yanataka uchaguzi ufanyike kwa njia ya posta ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19. Majimbo mengi yameruhusu mfumo huu wa upigaji kura kwa miaka kadhaa na hayajaripoti matatizo yoyote makubwa isipokuwa matukio madogo.

Chini ya uchaguzi wa urais, Bwana Trump hana mamlaka yoyote ya kuahirisha uchaguzi yeye binafsi na tukio kama hilo ni lazima liidhinishwe na bunge.

Bwana Trump alisema njia hiyo tayari unadhihirisha kwamba hilo litakuwa matatizo tu katika maeneo ambayo imejaribiwa.

Mapema mwezi huu, majimbo sita ya Marekani yalikuwa yanapanga kufanya uchaguzi wa Novemba kwa njia ya posta: California, Utah, Hawaii, Colorado, Oregon naWashington.

Majimbo hayo yatatuma kura moja kwa moja kwa njia ya posta kwa wapiga kura wote waliosajiliwa, na baada ya hapo zitarejeshwa tena au kuwasilishwa siku ya kupiga kura - ingawa kupiga kura moja kwa moja bado kutakuwepo kwa wachache ambao hali italazimu kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.