Pata taarifa kuu
CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: China yathibitisha visa vipya 105 vya maambukizi

China imerekodi visa vipya 105 vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyothibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, rekodi ya kila siku kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu, mamlaka ya afya nchini humo imesema.

Kulingana na takwimu rasmi, kesi 84,165 za maambukizi zimethibitishwa katika China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo, ambalo limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini kote.
Kulingana na takwimu rasmi, kesi 84,165 za maambukizi zimethibitishwa katika China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo, ambalo limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini kote. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kati ya kesi hizi mpya, 96 zimeripotiwa katika mkoa wa Xinjiang magharibi mwa nchi, ambapo kumezuka maambukizi mapya , Tume ya Kitaifa ya Afya imesema.

Kesi moja imethibitishwa Beijing, tume hiyo imebaini katika taarifa yake ya kila siku kuhusu janga la Covid-19.

Kulingana na takwimu rasmi, kesi 84,165 za maambukizi zimethibitishwa katika China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo, ambalo limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini kote. Hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Alhamisi.

Kwingineko duniani ambako idadi ya vifo inaendelea kutisha ni nchini Marekani na Brazil, ambapo nchi hizo zilizoathiriwa zaidi na janga la Corona zimethibitisha vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

Marekani imerekodi vifo zaidi ya 150,000, na Brazil kwa upande wake imethibitisha vifo 90,000 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.