Pata taarifa kuu
BOLIVIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchunguzi wa kimataifa kuhusu uchaguzi wa urais waanza Bolivia

Waangalizi wa kimataifa kutoka Jumuiya ya nchi za Amerika wameanza tangu Alhamisi, Oktoba 31, uchunguzi wao kuhusu uhesabuji wa matokeo ya uchaguzi wa urais, wakati makabiliano kati ya raia yamesababisha vifo vya watu wawili katika mji wa Santa Cruz.

Wafuasi wa Rais Morales waandamana katika mitaa ya La Paz, mji mkuu wa Bolivia, Oktoba 31, 2019.
Wafuasi wa Rais Morales waandamana katika mitaa ya La Paz, mji mkuu wa Bolivia, Oktoba 31, 2019. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Wataalam wa Jumuiya ya nchi za Amerika (OAS) wameanza Alhamisi hii uchunguzi wao juu ya uhesabuji wa kura za uchaguzi wa urais wa Oktoba 20.

Uchunguzi huu unafuatia makubaliano ya yaliyofikiwa kati ya serikali ya Bolivia na jumuiya hiyo yenye makao yake makuu jijini Washington, jumuiya ambayo inajumuisha serikali mbalimbali za mataifa ya Amerika.

"Leo ukaguzi huu unaanza, ambao utadumu takriban wiki mbili," Waziri wa Mambo ya Nje wa Bolivia, Diego Pary amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Uchaguzi ulikuwa wa wazi, uchaguzi ulifanyika kwa mujibu wa Katiba na sheria za Bolivia, lakini tumekubali jukumu la ujumbe wa ukaguzi wa Jumuiya ya nchi za Amerika, Diego Pary Waziri wa Mambo ya Nje wa Bolivia, amebaini alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu Natalia Olivares

Kuanza kwa zoezi hili la ukaguzi halita punguza mvutano kati ya wafuasi wa Evo Morales na wale wa upinzani.Siku ya Jumatano upinzani ulitangaza kwamba haukubaliani na uchunguzi huu kwa hali ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.