Pata taarifa kuu
BOLIVIA-UCHAGUZI-SIASA

Sintofahamu yatokea Bolivia, Carlos Mesa apinga matokeo ya uchaguzi wa urais

Wakati nchi inajiandaa kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliopangwa Desemba 15 kati ya rais anayemaliza muda wake Evo Morales, rais tangu mwaka 2006, na Carlos Mesa, rais wa zamani, mvutano wa kisiasa umeibuka.

Wafuasi wa mgombea Carlos Mesa, aliyefuzu katika duru ya pili ya uchaguzi, wapandwa na hasira baada ya Mahakama Kuu ya Uchaguzi kubadili matokeo ya uchaguzi.
Wafuasi wa mgombea Carlos Mesa, aliyefuzu katika duru ya pili ya uchaguzi, wapandwa na hasira baada ya Mahakama Kuu ya Uchaguzi kubadili matokeo ya uchaguzi. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Mahakama Kuu ya Uchaguzi nchini Bolivia (TSE) imetangaza kwamba Evo Marales anaongoza na anaweza kushinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Kauli ambayo inatofautiana na kauli yake ya kwanza.

Jumapili jioni, Oktoba 20, Mkuu wa Mahakama Kuu ya Uchaguzi, Maria Eugenia Choque, alitangaza Evo Morales alipata 45.28% ya kura na mpinzani wake Carlos Mesa akipata 38.16% ya kura, na hivyo wote wawili kupata nafasi ya kupambana katika duru ya pili, baada ya 84% ya kura kuhesabiwa.

Wakati huo tangazo la matokeo ya awali ya uchaguzi yalifutwa ghafla Jumapili usiku kwenye tovuti ya Mahakam Kuu ya Uchaguzi (TSE), bila maelezo. Kabla ya kurejea tena Jumatatu usku na kuhitimisha kwamba Morales amepata 46.87% kura dhidi ya mpinzani wake Mesa, ambaye amepata 36.73 ya kura, baada ya 95% ya kura kuhesabiwa.

Waangalizi kutoka nchi Jumuiya ya nchi za Amerika (OAS), waliopo Bolivia kwa uchaguzi wa rais, wameelezea "wasiwasi" kuona mahakam Kuu ya Uchaguzi inabadili kauli ya matokeo ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.