Pata taarifa kuu
MAREKANI-USAFIRI-AJALI-USALAMA

Marekani yasitisha safari za Boeing 737 MAX

Marekani pia imeamuru kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 na MAX 9. Hatua hiyo imechukuliwa Jumatano, Machi 13, hatua ambayo inakuja baada ya nchi nyingi barani Ulaya kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX.

Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la MArekani la American Airlines, ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Miami International, Florida Machi 13, 2019.
Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la MArekani la American Airlines, ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Miami International, Florida Machi 13, 2019. JOE RAEDLE / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili Machi 10, 2019 ajali ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la Ethiopia la Ethiopian Airlines iliua watu 157 kutoka mataifa 35 jijini Addis Ababa.

Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu wengi.

Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.

Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Marekani (FAA), imesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.

Awali rais Donald Trump alitangaza kwamba shirika la FAA litatoa tangazo la dharura kufuatia "taarifa mpya na ushahidi "kutoka eneo la mkasa na kutoka maeneo mengine kupitia malalamiko mengine tofauti'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.