Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-AJALI-USALAMA

Visanduku vyeusi vya Boeing 737 MAX vyapatikana

Hatimaye uchunguzi umeanza ili kujua sababu za ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines iliyotokea Jumapili tarehe 10 Machi, karibu na mji wa Addis Ababa, nchini Ethiopoia. Ajali hiyo imeua watu 157 kutoka mataifa 35 tofauti.

Sherehe ya kukabidhi ndege aina ya Boeing 737 MAX 8, katika kiwanda cha Boeing cha Zhoushan, Desemba 15, 2018.
Sherehe ya kukabidhi ndege aina ya Boeing 737 MAX 8, katika kiwanda cha Boeing cha Zhoushan, Desemba 15, 2018. © REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Wachunguzi kutoka Ethiopia na Marekani wanatarajia kutoa mwanga kuhusu ajali hiyo. Visanduku vyeusi viwili vinavyorekodi mawasiliano ndani ya ndege vimepatikana kwenye mabaki ya ndege hiyo leo Jumatatu, wakati safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX zimesitishwa nchini Ethiopia, Indonesia na China.

Hata hivyo visanduku hivyo hayajafanyiwa uchunguzi. Mpaka sasa, hajajulikana iwapo ndege ya hiyo ya shirika la ndege la Ethiopian ilianguka kutokana na kosa la kibinadamu, sababu kutoka nje au tatizo la kiufundi.

Lakini wengi wameanza kutilia mashaka ndege yenyewe na kuanza kujiuliza maswali mengi kuhusu safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX 8.

Mnamo mwezi Oktoba, ndege nyingine aina ya Boeing 737 MAX 8, ya shirika la ndege la Simba Air, alianguka katika Bahari ya Java, na kuua watu 189. Sababu ya ajali hiyo, iliyotokea muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, hazikuelezwa.

Kutokana na hali hiyo, mamlaka nchini China imeagiza mashirika ya ndege nchini humo kusitisha safari za ndege zao aina ya Boeing 737 MAX.

Mashirika ya ndege ya China yana ndege 96 aina ya Boeing 737 MAX, mamlaka imesema.

Gazeti la Caijing linaripoti kwamba safari nyingi za ndege zilizopangwa kutumiwa na ndege hizo hutumiwa na ndege aina ya Boeing 737-800.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.