Pata taarifa kuu
VENEZUELA-WAHAMIAJI-USALAMA

Nchi tatu za Kusini mwa Amerika zaomba msaada kukabiliana na wakimbizi

Nchi tatu za Kusini mw Amerika, Colombia, Peru na Ecuador zinaomba msaada zaidi wa kimataifa ili kukabiliana na ongezeka la wahamiaji kutoka Venezuela ambao wanazidi idara zao za huduma kwa umma, mwakilishi wa Peru amesema baada ya mkutano wa pamoja huko Lima kuhusu wahamiaji.

Wahamiaji wa Venezuela, njiani, wakielekea Ecuador, Agosti 21, 2018.
Wahamiaji wa Venezuela, njiani, wakielekea Ecuador, Agosti 21, 2018. REUTERS/Andres Rojas
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi tatu zimepokea mamia ya maelfu ya Wavenezuela wanaokimbia mdororo wa kiuchumi na kisiasa nchini mwao, ambako raia wamekua wakijiwezesha wenyewe kwa kupata chakula na kuondokana na matatizo ya maisha ya kila siku.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Wvenezuela zaidi ya milioni 1.6 wameitoroka nchi yao tangu mwaka 2015, ikiwa ni mojawapo ya wakimbizi wengi katika historia ya Amerika Kusini.

Juma lililopita, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ilitangaza kwamba idadi ya Wavenezuela wanaoikimbia nchi yao iko karibu kufikia kiwango cha "hatua ya mgogoro" sawa na suala la wahamiaji katika bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya.

Akiwa ziarani nchini Colombia siku ya Alhamisi, ambapo alikua anaendelea na ziara yake Kusini mwa Amerika, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez aliahidi kuwa Umoja wa Ulaya utatoa euro milioni 35 kusaidia eneo hilo kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.