Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MADURO-USALAMA

Maduro aapa kulipiza kisasi baada ya kuponea kuuawa

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, akiungwa mkono na jeshi, amesema anajiandaa kulipiza kisasi kwa kutumia mkono wa chuma dhidi ya shambulizi, ambalo anadai lilikua limemlenga.

Nicolas Maduro wakati shambulio lililopotokea alipokua akihutubia umati wa askari katika sherehe ya kijeshi, Caracas Agosti 4, 2018.
Nicolas Maduro wakati shambulio lililopotokea alipokua akihutubia umati wa askari katika sherehe ya kijeshi, Caracas Agosti 4, 2018. VENEZUELAN GOVERNMENT TV/Handout via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Upinzani unasema una hofu ya kutokea wimbi jipya la ukandamizaji.

Siku ya Jumapili Waziri wa Ulinzi Vladimir Padrino Lopez pamoja na mkuu wa majeshi, walitangaza kwamba wanamuunga mkono rais Maduro na wako tayari kumsaidia.

"Tunaendelea kujitolea kwa imani zetu, kwa kumuunga mkono bila kuficha amiri wetu mkuu wa jeshi," alisema waziri wa ulinzi wa Venezuela.

Alithibitisha madai ya Bw Maduro kwamba siku ya Jumamosi aliponea kuuawa katika shambulizi lililoendeshwa na ndege zisizokuwa na rubani zilizokua zilibeba vilipuzi wakati wa sherehe ya kijeshi katikati mwa mji mkuu Caracas.

Jeshi la Venezuela, ambalo lina nguvu kubwa za kisiasa na kiuchumi, linachukuliwa kuwa kiungo kikubwa katika kumsaidia Bw Maduro, ambaye pia amepoteza imani kwa raia kwa sababu ya mdororo wa kiuchumi unaoikabili nchi ya Venezuela.

Watu sita wanaoshutumiwa kujaribu kumuua Maduro wamekamatwa, Waziri wa Mambo ya Ndani Nestor Reverol alisema siku ya Jumapili.

Askari saba walijeruhiwa katika shambulio hilo, alisema.

"Hadi sasa tuna magaidi sita na ambao wamekamatwa, magari kadhaa yalimkamatwa, na msako uliendeshwa katika hoteli mbalimbali katika mji mkuu, ambapo kuna ushahidi tosha," alisema waziri huyo.

"Wahusika na waandaaji wa shambulizi hilo nje na ndani ya nchi wametambuliwa" na "kuna watu wengine wengi ambao watakamatwa katika saa chache zijazo," alisema Reverol.

Mwanasheria Mkuu Tarek Williams Saab, aliye karibu na utawala, ametangaza kwamba atataja Jumatatu wiki hii majina ya watu waliokamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.