Pata taarifa kuu
EU-VENEZUELA-VIKWAZO-UCHUMI

Umoja wa Ulaya watishia kuweka vikwazo vipya dhidi ya Venezuela

Federica Mogherini, msemaji wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, ameitishia Venezuela kuiwekea vikwazo vipya kama "hali ya mchakato wa uchaguzi wa kuaminika" haukuheshimiwa wakati wa Uchaguzi mkuu wa Mei 20."

Federica Mogherini msemaji wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya.
Federica Mogherini msemaji wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya utafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi na maendeleo yake na itakuwa tayari kujibu kwa hatua zinazofaa kwa uamuzi wowote au hatua ambayo inaweza kudhoofisha demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu, "amesema katika taarifa.

Umoja wa Ulaya, ambao unashutumu rais Nicolas Maduro kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, iliiwekea vikwazo Venezuela mnamo mwezi Novemba.

Rais Maduro anaendelea kukosolewa kwa hatua zake dhidi ya upinzani na amekua akishtumiwa kutaka kuitumbukiza Venezuela katika dimbwi la machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.