Pata taarifa kuu
GUATEMALA-VOLKANO-USALAMA

Guatemala: Idadi ya waliofariki kufuatia mlipuko wa volkano yafikia 69

Watu wasiopungua 62 wamefariki na wengine wengi wamejeruhiwa kufuatia mlipuko wa volkano uliotokea Jumapili, Juni 3 nchini Guatemala. Awali idara inayokabiliana na majanga nchini Guatemala ilitangaza kwamba watu zaidi ya 25 walipoteza maisha na 20 walijeruhiwa kufuatia mlipuko huo.

Maafisa wa Zima Moto katika mji wa San Juan Alotenango baada ya mlipuko wa volkano ya Fuego.
Maafisa wa Zima Moto katika mji wa San Juan Alotenango baada ya mlipuko wa volkano ya Fuego. REUTERS/Luis Echeverria
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya hapo serikali ya Guatemala ilisema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Mlipuko wa Volkano ya Fuego (Volkano ya moto), inayopatikana kilomita 35 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Guatemala, umesababisha maelfu ya watu kuhamishwa na uwanja wa ndege wa kimataifa umetakiwa kufungwa.

Askari wakisafisha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa La Aurora, Guatemala City tarehe 3 Juni 2018.
Askari wakisafisha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa La Aurora, Guatemala City tarehe 3 Juni 2018. REUTERS/Luis Vargas

Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Mlipuko huo umeathiri hasa wilaya za vijijini zilizo karibu na volkano hiyo na mji wa kikoloni wa Antigua, eneo muhimu kwa utalii nchini Guatemala.

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhari imetolewa.

Wakati huo huo Israeli imetangaza kwamba imetoa msaada wa dharura nchini Guatemala, wenye thamani ya Dola 10,000. Msaada huu, uliotumwa kupitia Ubalozi wa Israel nchini Guatemala, unajumuisha madawa, chakula na mablanketi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israeli imebaini kwenye vyombo vya habari vya kijamii.

"Volkano ya moto" ilianza kulipuka Guatemala, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 68 na maelfu ya watu wamehamishwa usiku wa Jumapili, Juni 3.
"Volkano ya moto" ilianza kulipuka Guatemala, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 68 na maelfu ya watu wamehamishwa usiku wa Jumapili, Juni 3. REUTERS/Luis Echeverria

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.