Pata taarifa kuu
MAREKANI

Siku 100 akiwa madarakani rais Trump aahidi mapambano zaidi

Rais wa Marekan Donald Trump amepongeza siku 100 za kuwepo kwake madarakani akisema zimezaa matunda huku akiwaambia maelfu ya wafuasi wake kuwa mapambano makubwa yaliyo mbele yao lazima wayashinde.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Akisoma hotuba yake ya muda mrefu iliyosheheni mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari na mtangulizi wake rais Barack Obama, huku akijisifu kuhusu kusaidia sekta ya kijeshi nchini Marekani, nafasi ya sera zake za kigeni ikiwa ni pamoja na kuikabili Korea Kaskazini, huku akisisitiza kauli yake ya kuifanya Marekani kuwa taifa kubwa tena Trump alishangiliwa na umati wuliokuwa ukimsikiliza huko Pennsylvania.

Hata hivyo wakati akiangaziwa bila kukoma tangu aishangaze dunia mwezi Novemba mwaka jana kwa ushindi ambao haukutarajiwa dhidi ya Hillary Clinton, rais Trump amejitahidi kutekeleza ahadi zake za kampeni bila mafanikio.

Jitihada zake za kufuta na kuchukua nafasi ya kihistoria ya mageuzi ya huduma za afya ya mtangulizi wake kuwa ziligonga mwamba katika bunge la Congress, ambapo idadi kubwa ya vipaumbele yake vya sheria vimekwamishwa na mchezo wa siasa baridi .

Aidha ufadhidli kwa ajili ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, uliondolewa kutoka muswada wa ufadhili wa serikali ili kuzuia kukwama kwa shughuli za serikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.